5/08/2021

Breaking: Sakata la Mtoto wa Amber Lulu, Harmorapa Akamatwa na Polisi

Msanii wa Bongo Fleva anayependa kiki Bongo, Hamorapa amekamatwa na polisi, leo Jumamosi, Mei 8, 2021, katika Ukumbi wa Hotel ya Kebbys, uliopo Mwenge, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

 

Kukamatwa kwa Harmorapa kunatokana na kauli yake aliyoitoa akidai kuwa mtoto wa Amber Lulu ni wa kwake kwani wanafanana.

 

Baada ya kauli hiyo mzazi mwenzake na Amber Lulu aanayejulikana kama Mr. Botion alimbana Harmorapa ambaye alikana na kusema kuwa mtoto huyo si wake.

 

lakini baada ya kuondoka alijirekodi tena kipande cha video akisema amenyanyaswa na kudharirishwa na Botion na wenzake hivyo akasisitiza kuwa mtoto yule ni wa kwake na atazungumza na wanahabari kuanika ukweli halisi, lakini wakati akiendelea kuzungumza na wanahabari ndipo Botion alitua na polisi wakamkamata na kumpeleka kituo cha polisi Mabatini.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger