Bunge laahirisha vikao vyake kufuatia kifo cha Mbunge Khatib Haji
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirisha vikao vyake vya leo mpaka kesho tena kufuatia kifo cha mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo Khatib Haji, aliyefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akitoa taarifa ya msiba huo leo Mei 20, 2021, Bungeni Dodoma, Naibu Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa mbunge huyo amefariki wakati akipatiwa matibabu na mazishi yanafanyika leo saa 10:00 jioni huko visiwani Pemba.

"Mh. Spika kwa masikitiko makubwa anawatangazia waheshimiwa wabunge kwamba mbunge mwenzetu Khatib Haji, mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo, amefarikia dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na mazishi yatafanyika leo Pemba, tutawakilishwa na wabunge wenzetu walioko Dar es Salaam", ameeleza Dkt Tulia Ackson


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE