Byabato Awaomba Radhi Watanzania Kisa Luku
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, amewaomba radhi Watanzanbia kufuatia tatizo la upatikanaji wa huduma ya LUKU lililojitokeza kwa siku ya nne leo na kudai kuwa wataalam wa TANESCO wamewaahidi hadi kufikia leo jioni tatizo hilo litakuwa limetatulika.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 19, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi, aliyehoji ni nini hatua za serikali kufuatia tatizo hilo ambalo linaikosesha TANESCO mapato pamoja na shughuli za wananchi kusimama.


“Toka asubuhi nimepokea simu na SMS nyingi sana kutoka kwa wananchi wakiuliza kwamba, wanashindwa kununua LUKU leo siku ya pili jambo ambalo linakosesha TANESCO mapato lakini shughuli za wananchi zinasimama, nini kauli ya serikali juu ya jambo hili,” ameshoji Cosato Chumi


Akijibu swali hilo, Byabato amesema; “Tumepata shida kubwa sana kwenye mfumo wa kidigitali wa kununua na kuuza LUKU lakini tunalishughulikia, tunaahidiwa na wataalamu wetu kabla siku ya leo haijaisha tatizo la LUKU litakuwa limeisha, niwaambie Watanzania wote kama ukifika ofisi za TANESCO unaweza ukanunua umeme, shida iliyopo ni kwenye mifumo ya kibenki na simu. Ninaomba radhi kwa niaba ya wenzangu.


“Tunaahidiwa na wataalamu wetu kabla siku ya leo haijaisha tatizo la LUKU litakuwa limeisha, niwaambie Watanzania wote kama ukifika ofisi za TANESCO unaweza ukanunua umeme, shida iliyopo ni kwenye mifumo ya kibenki na simu. Ninaomba radhi”-Stephen Byabato Naibu Waziri,” amesema Byabato.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE