Dalili zitakazokuonesha msichana anayekupenda ila anashindwa kukuambia

Kwa hivi sasa kumekuwapo na imani potofu kwa wanawake kwamba hawawezi kumwambia ukweli mwanaume anampenda kwanza mpaka mwanaume aanze lakini ukweli usiopingika ni kwamba wao pia hupendi na mara nyingi wao wakianza kupenda hupenda kweli kufikia hatua hata ya kuhisi kuumwa.Hizi ni dalili za mwanamke anaekupenda ila anagoma kukwambia tu;


Huwa anapenda kukugusa sehemu yako ya mwili. 
Haoni aibu kugusa sehemu ya mwili wako. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomasa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahishishia kazi ya kuwa na wewe.

Kupenda kucheka tena muda mwingine kwa nguvu 
Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli.

Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi na hupenda yale afanyiwe yeye tu hata kama sio mpenzi wako.

Hukumbuka matukio mengi yanayokuhusu wewe.
Anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifauli mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza.

Hupenda kuangaliana na wewe muda mwingi.
Eye contact hupendelea sana kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utamuelewa ni kiasi gani anakupenda kupitia vile anavyokuangalia. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda hivyo huweka jicho la wizi na kukuvizia.

Hupenda kukaa muda mwingi na wewe.
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe na akikaa na wewe hupendelea sana mwanzoni kukujua wewe zaidi na hukujengea mazingira ya wewe uwemuwazi ili umwambie mengi kuhusu wewe na pia akiwa na wewe atakuwa muwazi zaidi hadi mavazi aliyovaa hupenda sana kujua yako na kukuambia yake na hupenda kujua ni mavazi gani yeye akivaa anakuvutia zaidi na atajitahidi kuwa anavaa ya style hiyo kukufurahisha.

Hupenda kutatua mikwaruzano yenu kwa amani 
Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia nakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikitokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.

Hupenda kukununulia zawadi za mitego 
Mwanamke anaekupenda hupenda kujua mengi sana kuhusu wewe na hapo inamsaiia kukununulia zawadi za mitego kama boxer , na mara nyingi hupenda rangi nyeupe, au kukununulia perfume , sabuni ya kuoge ya manukato,soksi, vest, bukta, saa,raba, t-shirt. Na kama mkitoka wote mkaenda shopping ataakutega kwa kukuonyesha vitu na wewe ukionekana umependa kitu hatonunua siku hiyo ila atanunua siku inayofuata na kukuletea kama suprise.

Kupenda mle wote 
Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi hupendelea msosi mle sehemu mmoja na kama ikitokea mwanaume hawezi kuhama sehemu anayokula mwanamke yupo radhi kubadili na kumfuata mwanaume hatakama sehemu hiyo yeye haipendi na kama unakula kwako basi atakutega na kuja kupika kwako ili mle na atakuwa anapenda kununua vitu vya kupika ili tu akutekena uone upendo wake.

NB: Kuwa makini, sio kila mwanamke atakaye onesha dalili hizi anakupenda kwa dhati, wengine hutaka kukuweka mtu kati ili akugagadue mpunga wako.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE