Diamond Platnumz Awapiga Mkwara Mzito FORBES Kuhusu Utajiri Wake "Nendeni Mkanigoogle"


Star wa muziki barani Afrika @diamondplatnumz ameshindwa Kulikalia Kimya swala la @forbes katika List ya Wasanii wa Afrika ambao wana Mkwanaj Mrefu zaidi kwa Sasa


Hatua hii inakuja baada ya hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari kutoa list (orodha) ya wasanii matajiri zaidi barani Afrika kwa kulihusisha jarida hilo la #Forbes


Katika taarifa hizo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyohusu wasanii 10 wanaoongoza kwa utajiri barani Afrika, huku zikimtaja @diamondplatnumz kukosekana katika orodha hiyo


Kupitia ukurasa wa instagram wa Star huyu amethibitisha taarifa hii kwa kuchapisha ujumbe baada ya kuonekana kusaini dili na kampuni ya kimataifa ya muziki duniani @warnermusic


Katika ujumbe huo @diamondplatnumz ameoneshwa kuulani utaratibu wa jarida hilo na kuwakumbusha kuwa safari nyingine wamfuatilie kiundani zaidi kwenye mtandao wa #Google


Forbes ni jarida la biashara la Kimarekani linalochapishwa kila wiki mbili likiangazia masuala ya fedha, viwanda, uwekezaji na masoko.


Forbes pia linaripoti kuhusu mada zinazofanana kama teknolojia, mawasiliano na siasa, makao yake makuu yako Jersey City, katika jimbo la New Jersey.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE