Dube Amgomea Kagere Bongo
MSHAMBULIAJI tegemeo ndani ya kikosi cha Azam FC, Prince Dube raia wa Zimbabwe amesema atazidi kupambania ndoto zake za kuwa mfungaji bora msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.

 

Dube ameyasema hayo baada ya kufikisha mabao 12 na kuwa kinara akimzidi bao moja Meddie Kagere wa Simba.

 

Kwa misimu miwili mfululizo, Kagere amefanikiwa kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora katika Ligi Kuu Bara na msimu huu anaifukuzia kwa mara ya tatu. 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Dube alisema: “Nawashukuru wachezaji wenzangu kwani mara zote wamekuwa wakinipa nafasi mimi ya kufunga na kunisogeza karibu na ndoto zangu.

 

“Ni ndoto yangu kuwa mfungaji bora ila nikiikosa basi nitahakikisha naisaidia timu yangu kufanya vizuri kwa kila mechi na nitakapopata nafasi ya kufunga basi nitaitumia vizuri.”

STORI NA CAREEN OSCAR, Dar es Salaam


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad