5/10/2021

Esma, Petit Man Majanga TenaDADA wa msanii mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan na mzazi mwenzie Hamad Manungwi ‘Petitman Wakuache’ wameingia kwenye majanga tena baada ya kudaiwa kuwa wamemwagana kwa mara ya nne, RISASI limenasa mchapo!Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa, wawili hao hawako pamoja kwani hawajaonekana pamoja muda mrefu.

 

“Ni muda sana sijawaona Esma na Petit kwa vyovyote vile watakuwa tayari wameshaachana maana nawajua wale, ukiona ukimya tu ujue jini mkata kamba kashafanya yake,” kilisema chanzo hicho.

 

Akizungumza na RISASI JUMAMOSI, mtu wa karibu na familia ya Esma, alisema wawili hao hawaonekani pamoja tena kama ilivyokuwa siku za nyuma kidogo na hata katika sherehe ya kuzaliwa mtoto wao Taraj, kila mmoja amemsherekea mtoto huyo kivyake.

 

“Sasa hivi Esma na Petit Man hawako pamoja na ninasikia kuwa Petit ana mwanamke mwingine ambaye anatarajia kujifungua wakati wowote na hata ukiangalia sherehe ya mtoto wao kila mtu kamfanyia kivyake maana mama yake kamfanyia dua na kufuturisha na baba yake kafanya hivyo akiwa nchini Afrika Kusini kawaagiza watu huku Bongo, wakawafuturisha watoto yatima na wakampelekea zawadi shule,” alisema mtu huyo.

 

Esma na Petitman tangu wafunge ndoa yao miaka sita iliyopita washaachana na kurudiana zaidi ya mara nne huku kila mmoja akiolewa na mwingine kuoa na wote kuwaacha wenza wao na kurudiana na sasa wameachana tena rasmi.

 

Mara ya mwisho Esma aliolewa na jamaa mmoja anayefahamika kwa jina la Msizwa kwa sherehe kubwa iliyohudhuriwa na mastaa wakubwa Bongo akiwemo Diamond Platnumz lakini hata hivyo, ndoa hiyo iliweka rekodi ya aina yake kwa kudumu muda mfupi sana.Baadaye, Esma alirejea kwa mara nyingine kwa Petit ambaye naye alikuwa ametoka kuachana na mwanamke wake waliyekuwa wakijiachia naye sana mitandaoni.

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI

O
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger