.

5/25/2021

Gari la rais wa Marekani latajwa kuwa gari salama zaidi duniani

Gari la rais wa Marekani kwa jina maarufu ''The Beast'' limetajwa kuwa gari salama zaidi duniani.
Gari hilo aina ya Cadillac lenye uzito wa takriban kilo 9000 ambalo kila mara rais anapokuwa katika ziara ya kigeni husafiriswa na ndege ya Airfoce One na kusimamiwa na kitengo cha ujasusi cha Marekani limedaiwa kumiliki vipengele vinavyoweza kumlinda rais wa taifa hilo lenye uwezo mkubwa duniani iwapo kutatokea shambulizi.

Gari hilo limeundwa kwa kutumia vyuma vilivyochanganywa na aluminium, titanium na ceramic vyenye uzito wa nchi sita kuzuia risasi yoyote kuingia.

Mwili wa gari hilo wenye uzito wa nchi sita una uwezo wa kuhimili shambulio la bomu.

Milango ya gari hilo, ina uzito wa nchi 8. Inapofungwa ina uwezo wa kuwalinda asilimia 100 wale walio ndani ya gari hilo iwapo kutatokea shambulio la kemikali.

Milango hiyo pia inaweza kuwekwa umeme ili kuwazuia wanaotaka kuingia kwa lazima.

Shina la gari hilo limejengwa na chuma kinachoweza kulilinda dhidi ya shambulio la bomu.

Matairi yake hayawezi kupata pancha au kutoboka yakiwa na chuma ndani yake.

Hatua hiyo huliwezesha gari hilo kuendelea na safari yake hata iwapo matari hayo yameharibiwa.

Kwa upande wa nyuma gari hilo lina uwezo wa kumwaga mafuta yanayoteleza barabarani ili kuyakosesha udhibiti magari yanayolifukuza.

Eneo la ndani ya gari la ''The Beast'' linimiliki vipengele kadhaa vya kujilinda , ikiwemo kipengee kimoja ambacho kinaweza kukwepa shambulio la kemikali kulingana na Reuters.

Eneo la nyuma la gari hilo ndilo ambalo rais na abiria wengine wanne hukaa. Likiwa limezibwa kwa glasi.

Kiti cha rais kilichopo nyuma ya gari hilo kinamiliki simu ya setlaiti yenye mawasiliano ya moja kwa moja na makamu wa rais wa taifa hilo na makao makuu ya ulinzi The Pentagon.

Tangi la mafuta la gari hilo limejengwa na mabati ambayo yanaweza kuzuia shambulio na kujazwa mapovu maalum ambayo yanalizuia gari hilo kulipuka iwapo litahusika katika ajali.

Eneo la nyuma la gari hilo {Boot} lina mfumo wa kukabiliana na moto ,vitoa machozi , na linaweza kutoa skrini yenye moshi .

Vilevile gari hilo lina dereva ambaye amepata mafunzo maalum kuweza kukabiliana na hali ya kutatanisha na kutoroka na rais .

Gari hilo pia linamiliki bunduki fupi na bomba la kutoa gesi ya kutoa machozi.

Mifuko ya aina ya damu ya rais pia huwa ndani ya gari hilo iwapo atahitaji kuwekwa damu.

Eneo la mbele la dereva lina kituo cha mawasiliano na mfumo wa ufuatiliaji wa GPS.

Vilevile kuna kamera iliofichwa inayoweza kuona nyakati za usiku.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger