Gwajima Atema Nyongo "Nchi ni Lazima IWE na Maono Kwa Ajili ya MIAKA Mingi Badala ya Ilani za Vyama vya Siasa"

advertise here

 


Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima amesema kwa sasa Tanzania haina maono ya muda mrefu kwaajili ya Maendeleo ya Wananchi bali kuna Ilani za Vyama na mipango ya muda mfupi


Amefafanua kuwepo kwa maono ya muda mrefu kutasaidia hata kumpima Rais anapoingia Madarakani kwa namna ambavyo anayatekeleza maono yaliyowekwa ila kwasasa tunaona tunasogea lakini ni kwa maono ya kila Serikali mpya inapoingia Madarakani


Ameongeza "Sasa hivi hatuna Vision bali tuna mambo ya kukimbiza. Kila Mwaka tunatafuta Madawati, kwani hakuna tawimu za kuonesha Mwaka huu tunahitaji Madawati mangapi kutokana na idadi ya Wanafunzi?".

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE