.

5/24/2021

Harmo Alimasha Dude Kila Kona..Wakenya Wadai Anajikosha
MWANAMUZIKI wa Tanzania, Rajab Abdul ‘Harmonize’, ameendelea kuliamsha dude kila kona. Baada ya kuliamsha na wasanii wenzake Bongo kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Dogo Janja na wengine, safari hii ameliamsha tena huko nchini Kenya.


Harmonize au Harmo ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Worldwide, amejikuta akishambuliwa mno baada ya kutoa kauli iliyowaudhi baadhi ya mashabiki wa muziki nchini Kenya.


Harmo amedai kwamba, muziki wa Kenya na Afrika Mashariki kwa jumla hauna viwango ndiyo maana haupenyi kimataifa kama ilivyo kwa muziki wan chi nyingine kama Nigeria, Afrika Kusini na kwingineko.


Kwa mujibu wa Harmo, wasanii kutoka nchini humo na ukanda mzima wa Afrika Mashariki wasipobadilika wataendelea kusindikiza wengine na kulalamika kila kukicha.Harmo anasema kuwa, kwa sasa, muziki wa Afrika Mashariki upo mbali mno kuweza kuchukua nafasi kwenye muziki wa Afrika.


Harmo ambaye ametua Bongo kwa mbwembwe juzi akitokea Lagos nchini Nigeria ambapo akiwa huko kwa takribani wiki mbili alidai kuwa, akiwa huko alisikia nyimbo chache mno za wasanii wa Afrika Mashariki zikipigwa kwenye redio na kumbi za starehe za usiku.


Alikwenda mbele zaidi na kusema kuwa, hata wimbo wake wa Attitude aliomshirikisha mwanamuziki wa Kongo, Awilo Longomba na H Baba ambao kwa sasa unatrendi kwa Afrika Mashariki, hata wenyewe haufanyi vizuri.


Anasema kuwa, wimbo wake wa Kainama aliomshirikisha Diamond Platnumz na Burna Boy, wenyewe unaendelea kufanya vizuri kwa nchi za Afrika Magharibi.


Kwa hiyo, Harmo anawataka wasanii wa Afrika Mashariki kuacha kujidanganya wenyewe.Kufuatia povu hilo la Harmo, baadhi ya wadau nchini Kenya wameendelea kutoa maoni mbalimbali juu ya kauli hiyo huku wengine wakidai kwamba anajikosha kama lilivyo jina la wimbo wake wa Anajikosha.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger