Harmonize, Mzazi Mwenziye Wakinukisha!




MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ kuonekana na mzazi mwenziye Shanteel.

 

Wawili hao walizua gumzo la aina yake baada ya kudaiwa kuonekana kwenye viunga vya Mlimani City jijini Dar, wakifanya shopping maalum kwa ajili ya mtoto wao, Zuuh.

akiwa amembeba mwanaye huyo wakizunguka kwenye moja ya maduka yaliyopo Mlimani City.

 

GUMZO LA SILAHA

Kuna video moja iliyodaiwa kuwa ilivuja, ilimuonesha Harmonize akiwa na silaha pale alipokuwa akitaka kumbeba mtoto wake akiwa kwenye maduka hayo lakini hata hivyo inasemekana aliifuta haraka.Kipande kingine, kilimuonesha Shanteel naye akiwa kwenye maduka hayo akiwa pia na mtoto wao huyo wakionekana kufanya manunuzi ya hapa na pale.RISASI pia litembelea kwenye Insta Story ya Shanteel na kujionea mazagazaga ambayo walimnunulia mtoto wao akiwa nyumbani.



CHANZO CHANENA

Kikizungumza na RISASI chanzo makini kilieleza kuwa, Harmonize sasa hivi anaweza kurudisha majeshi muda wowote kwa mzazi mwenziye huyo kwani hana mtu baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba wake, muigizaji Kajala Masanja.“Mtalaka bwana hatongozwi lolote linaweza kutokea Konde Boy hana baya kwa Shanteel, anaweza akafanya jambo na mambo yakawa vizuri,” kilisema chanzo makini.

 

MITANDAONI SASA

Mbali na chanzo hicho, mitandaoni kulikuwa na gumzo kama lote la kumtaka Harmonize arejeshe majeshi kwa mzazi mwenziye huyo huku wengi wakisema eti wanaendana zaidi kuliko Kajala.“Mambo si ndio haya sasa jini mkata kamba akafie mbali na *** yake kama mitungi ya mbege,” aliandika Instasihami6 kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

“Konde aoe huyo mwanamke awali ni awali hakuna awali mbovu mtoto apate malezi ya baba na mama,” aliandika Gracesarakikyaa Instagram.

 

“Wamependeza sana kwa nini Harmonize asimuoe huyu walee mtoto wao,” aliandika Am.ina5090.Maoni mengine kwenye kurasa mbalimbali za Instagram yalikuwa yakimgusa mke wa Harmonize Sarah ambaye aliwahi kudai mtoto huyo si wa Shanteel lakini hata hivyo wengi hawakutaka kuyaunga mkono zaidi ya kumtaka Harmonize arudishe majeshi.



TUJIKUMBUSHE

Harmonize aliachana na mkewe Sarah kisha kukita nanga kwa Kajala ambaye walidumu kwa takriban miezi isiyozidi mitatu kisha kumwagana.Sababu za kumwagana kwa Harmonize na Kajala ni madai ya staa huyo wa Bongo Fleva kutaka kumuomba penzi mtoto wa Kajala, Paula.

 

Baada ya Kajala kushtukia mchezo huo na kunasa baadhi ya meseji na picha za faragha, aliamua kuachana naye mazima kisha baadaye picha hizo za faragha za Harmonize kusambazwa na watu mbalimbali akiwemo hasimu wake, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’.

 

Harmonize alilifikisha suala hilo polisi na watu mbalimbali waliitwa na kuhojiwa lakini mpaka sasa polisi wamekuwa kimya, hawaelezi nini hatma ya jambo hilo zaidi ya kusema uchunguzi unaendelea.
 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE