.

5/29/2021

Hatimaye Dulla Makabila Afunga ndoa na Mrembo HuyuStaa wa muziki wa singeli nchini, msanii Dulla Makabila siku ya Alhamisi, Mei 27, alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Bi. Rahma Waziri, maeneo ya Kawe Beach, Jijini Dar es salaam.

Harusi ya wawili hao ilirushwa Live kupitia BONA Tv ambapo pia walifanyiwa mahojiano na kituo hicho.

Rahma Waziri ambaye ndiye mke wa Dulla Makabila alielezea kwamba alimjua #Dulla miaka 8 iliyopita na uhusiano wao umekuwa wa kuachana na kurudiana mara nying hadi sasa walipoamua kuwa mke na mume.

Rahma alijitambulisha kuwa ni mhudumu wa afya (Nesi) ambaye anaishi na kufanya kazi Marekani na alirejea hapa nchini yapata siku tano zilizopita kwa ajili ya harusi hiyo.

Alipoulizwa ikiwa atamkubalia Dulla Makabila (mume wake) aoe mke wa pili, #Rahma alisema hilo halipo na tayari wameshajadili kuhusu hilo.

Dulla naye alisema watasikilizana na kupanga namna gani watakuwa wanatembeleana kabla ya kuamua pa kuishi kabisa kama ni Tanzania au Marekani.

Sanjali na hilo, Dulla Makabila alilalamika kuhusu wasanii ambao walikausha kutoa michango kwa ajli ya harusi yake, akisema kuwa ameshawatungia nyimbo na ataitoa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Dulla Makabila, wasanii hao hawakuamini kwamba anaoa kweli ila walidhania anachangisha tu pesa kwa sababu nyingine akisingizia ndoa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger