Huu Ndiyo Undani wa Utapeli wa lambalamba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Wananchi wa Kijiji cha Mawenzusi, Sumbawanga mkoni Rukwa, wamelalamikia utapeli unaofanywa na waganga wanaojiita lambalamba wanaopita majumbani na kuwaaminisha kuwa wamewekewa vitu vya kishirikina na mahasidi wao na wakiingia ndani hufukia vitu vyao na kisha kuvitoa na kutaka walipwe.

 

Wananchi hao wametoa kero hiyo mbele ya mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfani Haule, mara baada ya kuwatembelea katika kijiji hicho alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo huku mwenyekiti wa kijiji hicho akikiri kushindwa kudhibiti utapeli huo.


"Nimekaa kupinga vitendo hivyo mpaka nimekaliwa vikao na vijana kiasi kwamba hata kutembea kwangu ni kwa wasiwasi", ameeleza mmoja wa wananchi hao


"Suala la lambalamba ni tatizo sana hapa kijijini ninaomba msaada wa kufa na kupona, niokolewe kwa sababu itafika wakati madhara yatatokea na itaonekana kwamba mimi Mwenyekiti ninahusika", ameeleza Mwenyekiti wa Kijiji hicho

 

Naye mwenyekiti wa waganga wa tiba asili mkoani Rukwa, Michael Jackson, amekemea vikali suala hilo huku akisema kuwa suala hilo halitambuliki kwa mujibu wa sheria zao na hivyo kinachofanywa ni wizi na utapeli kwani hawana vibali.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa watu hao wamepita kila vijiji vya wilaya hiyo na baadhi yao wamekwishakamatwa hivyo serikali itawachukulia hatua na mkondo wa sheria lazima ufuatwe

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad