ICC yamhukumu kiongozi wa zamani wa LRA Dominic Ongwen kifungo cha miaka 25


Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imemhukumu kifungo cha miaka 25 kiongozi wa zamani wa waasi wa Lord's Resistance Army,LRA Dominic Ongwen.
Dominic Ongwen, anayefahamika kama White Ant, alipatikana na zaidi ya makosa 60 ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw. Ongwen amepewa adhabu ndogo kwasababu alikuwa ametekwa na LRA akiwa mtoto mdogo.

Kundi hilo la waasi liliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ikiendesha shughuli zake nchini Uganda na mataifa jirani.

Dominic Ogwen alizaliwa mwaka 1975 katika kijiji cha Choorum wilaya ya Amuru kaskazini mwa Uganda.

Alitekwenyara na kundi la waasi wa Josephy Kony akiwa mvulana mdogo wakati akielekea shule ya msingi Abili Koro, kulingana na maelezo yake alidai alitekwanyara mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 14.

Lakini ripoti sahihi zinasemekana alitekwanyara akiwa na umri wa miaka 9 au 10.

Kwani alibebwa katika safari yao hadi kwenye kambi ya LRA, alikuwa hawezi kutembea.

Mama yake Ogwen alipofahamishwa habari za kutekanywara kwa mtoto wake aliamuwa kuwafata wafuasi hao, na badaye watu walimkuta mama huyo amefariki pamoja na mumewe.

Baada ya muda akiwa na umri wa miaka 18, Ogwen alipewa cheo cha Brigadier wa kundi la waasi wa LRA na kuongoza kikosi cha Sinia.

Ogwen alishirika katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa kivita mwezi wa Mei mwaka 2004 walishambulia kambi ya ndani ya Lukodi wilayani Gulu kaskazini mwa Uganda.

Pia alishambulia kambi nyingine za ndani ikiwemo ya Pajule, Odeke na Abok na kushiriki mauaji mbalimbali ya wanchi wasiokuwa na hatia , ubakaji na unyanyasaji wa kigono.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE