IGP Sirro: Hali ya Usalama ni Shwari, Makusanyo Yamepungua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amesema hali ya usalama nchini ni shwari, na hakuna matukio ya kutisha. IGP Sirro ametoa kauli hiyo katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua kiwanda cha ushonaji cha Jeshi la Polisi.

 

Amesema kuna matukio madogo ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitokea katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo Jeshi la Polisi nchini limekuwa likikabiliana nayo.

 

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini amesema matukio ya uhalifu nchini yameendelea kupungua, na kutolea mfano katika kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu yamepungua kwa zaidi ya asilimia 13 tofauti na ilivyokuwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

 

Amesema katika kipindi hicho hicho, pia ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 29.1. Kwa mujibu wa IGP Sirro, Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ndani na nje ya nchi, linaendelea kupambana na vitendo vya ugadi na biashara ya dawa za kulevya.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro amesema kiwango cha makusanyo ya faini za makosa ya Barabarani kimepungua kwasababu Watu wengi sasa wanaanza kuwa watii; “Mwaka jana July 2019 na July 2020 jumla ya Tsh. Bilioni 56 zilikusanywa lakini sasa kiwango kimepungua.

 

Tumekubaliana kwamba lazima makosa makubwa tuwe tumekamilisha upelelezi kwa miaka 2 na makosa madogo angalau kwa miezi sita, nikuhakikishie Mh. Rais kwamba suala la mrundikano mahabusu na uchelewashwaji wa kesi litaendelea kupungua.

 

“Hali ya ulinzi na usalama wa nchi yetu inaridhisha sana hatuna matukio makubwa ya kutisha ila tuna matukio madogo madogo ya uvunjaji na ukabaji, bado tuna changamoto ya matukio yanayovuka mipaka kama madawa ya kulevya na ugaidi.

 

“Tumeendelea kukusanya tozo za usalama barabarani na hii huwa tunapata changamoto kwani baadhi ya wananchi huwa wanalalamika labda sisi ni wakusanya kodi, hapana sisi huwa tunasimamia sheria na sheria inapovunjwa tunazidi kukusanya zaidi,” amesema Sirro.

 

Aidha, kuhusu nidhani ndani ya Jeshi la Polisi, IGP Sirro amesema ni ya kuridhisha na askari ambao wamekuwa wakikiuka sheria wanachukuliwa hatua za kinidhamu.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad