.

5/25/2021

INATISHA: Watu Wasiojulikana Wafukua Mwili wa Marehemu

 


Watu wasiojulikana wamefukua mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Rehema Michel aliyefariki kwa ajali ya gari, tarehe 23/05/2021, na kuchukua baadhi ya viungo vya mwili huo ikiwemo kichwa, sehemu za siri, mapafu, moyo, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kutokomea navyo kusikojul


Tukio hilo ambalo limeleta taharuki na simazi kubwa miongoni mwa wanakijiji limetokea jana katika   kijiji cha Nguyami, kata Idibo  wilayani Gairo mkoani Morogoro na kuwaacha watu wengi wakiwa na maswali hususan ndugu wa marehemu kwani wamehindwa kutambua nini lengo la watu hao.

Akielezea tukio hilo ndugu wa marehemu Binifasi Masaly amesema juzi tu walipata taarifa ya kuondokewa na ndugu huyo ambapo mwili waliuleta juzi na kuuzika majira ya saa sita huku wakifuata taratibu zote za kimila, lakini jana asubuhi wamekuja kujuzwa juu ya tukio la kufukiliwa kwa kaburi la ndugu yao na walipopata kibali cha serikali cha kukagua kaburi hilo ndipo walipogundua kuwa baadhi ya viungo havipo.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Nchembe mbali na kusikitishwa na tukio hilo la kikatili lililoibua simanzi upya na taharuki kwa wakazi wa eneo hilo, amekemea vikali vitendo vya ushirikina katika wilaya yake.

“Hili ni tukio baya kuliko matukio yote nimewahi kuyaona kwa macho yangu, mwili wa marehemu umenyofolewa viungo, kichwa kimekatwa, wamechukua sehemu za siri, kifuani wamepasua wakachukua moyo, kwa kwa kweli jambo hili linahuzunisha sana, na moja kwa moja linaoanishwa na imani za kishirikina,” amsema Bi. Siriel.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger