Jack Wolper Aonesha Ujauzito Wake na Rich Mitindo


Hatimaye staa wa filamu nchini @wolperstylish na mpenzi wake @richmitindo wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza

Hii inafuata baada ya kusambaa kwa picha iliyowekwa mtandaoni, na mwandani wake huyo (@richmitindo)kwenye ukurasa wake wa instagram ikimuonesha #Wolper akiwa na ujauzito, na kusindikiza ujumbe ulioashiria kuwa amejawa na furaha isioelezeka

"Sijuii nieleze vip Furaha yangu, Ila ni wakati mzuri na sitausahau kamwe kwenye maisha yangu.. jamaniii katika maisha yangu sijawahi kuwa na furaha na upendo kamili Kama ilivyokuwa wakati huu niseme nakupenda kuliko chochote katika ulimwengu huu, ilikuwa ndoto yangu kuwa na familia na sasa inatimia, kwa hili nitashukuru milele Nakupenda Jacq wangu na nitampenda mwanangu sana sababu umembeba mwanangu ndani yako, nakuhahid nitakuwa baba bora mwaminifu kwako na mwenye upendo , na nitakuwepo na nyie milele šŸ™ @wolperstylish" ✍️....@richmitindo

Inasemekana wawili hawa wanatajwa kuwa pamoja katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE