.

5/22/2021

Jackline Asisitiza ‘Mzee Mengi Hakuwa Mwendawazimu’

MJANE wa Marehemu Reginald Mengi, Jackline Ntuyabaliwe ameonesha kutorodhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu mumewe.

 

Aliandika katika mtandao wake wa Instagram: “Imetosha…. Ripoti ya matibabu ya Dkt. Reginald Mengi imeambatanishwa kama ushahidi. Ukweli kwa wale wanaopenda ukweli. Mume wangu alitumia maisha yake yote kama mtu anayeheshimiwa, mwerevu mkarimu na msaidizi kwa maelfu ya Watanzania. Hakuwa mwendawazimu! Unaweza kusema chochote unachotaka na uchukue kila kitu lakini kwa hili nitamtetea mpaka kifo.

 

Aliandika katika mtandao huo akiambatanisha ripoti ya daktari wake aliyetoa mapendekezo kuhusu afya ya marehemu, kuwa ugonjwa wa kiharusi alioupata haukuathiri uwezo wake wa kiakili.

 

Mahakama ilisema nini?

Siku chache zilizopita akisoma hukumu yenye kurasa 72, Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt Mengi ulioandikwa tarehe 17 mwezi Agosti mwaka 2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.

 

Katika shauri hilo watoto wa Marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na marehemu baba yao na saini iliyopo kwenye wosia ni tofauti na sahihi nyingine za marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.

 

Watoto wakubwa wa marehemu walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria kwasababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger