Jackline Mengi apinga hukumu "Imetosha marehemu mumewe hakuwa mwendawazimu"

advertise hereMjane wa Marehemu Reginald Mengi, Jackline Ntuyabaliwe ameonesha kutorodhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu mumewe.
Aliandika katika mtandao wake wa Instagram:

''Imetosha.... Ripoti ya matibabu ya Dk Reginald Mengi imeambatanishwa kama ushahidi. Ukweli kwa wale wanaopenda ukweli. Mume wangu alitumia maisha yake yote kama mtu anayeheshimiwa, mwerevu mkarimu na msaidizi kwa maelfu ya Watanzania''. Aliandika Jackline.

Hakuwa mwendawazimu! Unaweza kusema chochote unachotaka na uchukue kila kitu lakini kwa hili nitamtetea mpaka kifo.

Aliandika katika mtandao huo akiambatanisha ripoti ya daktari wake aliyetoa mapendekezo kuhusu afya ya marehemu, kuwa ugonjwa wa kiharusi alioupata haukuathiri uwezo wake wa kiakili.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE