John Cena ameomba radhi China kwa kutambua Taiwan kama nchi

 
Nyota wa WWE John Cena ameomba radhi China kwa kutambua Taiwan kama nchi.

Muigizaji huyo na mwanamieleka wa zamani wa WWE alitaja Taiwan kuwa nchi katika video ya biashara ya filamu ya hivi punde ya Fast and Furious.

Hatua hiyo iliikasirisha China ambayo inachukulia Taiwan inayojitawala kuwa chini ya himaya yake.

Bwana Cena ameweka video nyingike katika mitandao ya kijamii akizungumza Kichina kuomba radhi kwa “kosa” hilo.

Utata ulianza wakati Bwana Cena aliposema Taiwan itakuwa “nchi” ya kwanza kuweza kutazama Fast and Furious 9, katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Taiwan TVBS (kwa Kichina).

Jumanne, Bw Cena alichapisha video kwenye wavuti ya Wachina ya Weibo, akiomba msamaha kwa “kosa” hilo.

 


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE