Kauli ya Jeshi la Polisi kuelekea Kariakoo Derby

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga kuimarisha usalama katika mechi ya Watani wa Jadi Simba dhidi ya Yanga Mei 8, 2021 katika Dimba la Benjamini Mkapa. 

Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa ametoa rai kwa wazazi wanaopenda kwenda na Watoto uwanjani kuwa makini na kutoruhusu Watoto kuzagaa uwanjani na kupelelea kupotea.

Katika hatua nyingine amewataka mashabiki na wapenzi wa vilabu hivyo kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa amani katika mchezo huo na endapo watakiuka sheria hawatosita kuwawajibisha.

“Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha usalama katika mtanange huo wa watani wa jadi, tunasisitiza utulivu na kutovunjwa kwa sheria kwakuwa tutakuwa kazini hatutosita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekuwa na viashiria vya kuvuruga utaratibu na sheria”, amesema Kamanda Mambosasa.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE