Kavejuru CCM Ashinda Ubunge Buhigwe
Felix Kavejuru (CCM) ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Buhigwe uliofanyika jana Jumapili Mei 16, 2021.

 

Akitangaza matokeo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 17, 2021 msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Marrycelina Mbehoma amesema Kavejuru amepata kura 25,274 akifuatiwa na mgombea wa ACT-Wazalendo, Garula Tanditse aliyepata kura 4,749.

 

Amebainisha wapiga kura walioandikishwa ni 112,333 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 30,713. Amesema kura halali zilikuwa 30,320 na zilizoharibika 593.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE