Kesi ya rushwa dhidi Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, akanusha mashtaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Kesi ya ufisadi dhidi ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma inatarajiwa kuanza leo, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.



Kiongozi huyo ambaye wakati mmoja aliwahi kusherehekewa kwa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kukana mashtaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa silaha miaka ya 1990.

Alidai kuwa mwathiriwa wa hujuma za kisiasa- na kwamba mahakama nchini humo zinashirikiana na mahasimu wake wa kisiasa.

Bwana Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.

Waafrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.

Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini waliohai wamemshtumu Bw. Zuma– kumlinganisha na jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad