Kigogo wa Tehama Tanesco Yamkuta

advertise here
WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemsimamisha kazi kwa siku kumi Meneja wa Tehama na huduma za biashara wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lonus Feruzi na wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau, ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za Kielekroniki.

 

Dkt. Kalemani amewaambia Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kuwa, endapo maelezo yao hayatajitosheleza Watumishi hao waondolewe kazini.

 

Kwa muda wa takribani siku tatu, wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia.ya Kielekroniki, na hivyo kulilazimu shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za mikoa na wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE