.

5/21/2021

Kijana mbaroni kwa tuhuma ya mauaji kisa wivu wa mapenzi Ruvuma

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Alfred Nombo (28) kwa kosa la kumuua Erasto Nchimbi (28) mkazi wa Kijiji cha Sara Wilayani Mbinga kwa kumchoma na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea May 19 mwaka huu majira ya Saa 4 asubuhi.

Amesema kuwa Nombo alikuwa na wivu wa kimapenzi kwa mke wa Nchimbi na kuamua kumuua kwa kumchoma na kisu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Maigwa amesema kuwa Nombo alinogewa na mapenzi ya mke wa marehemu Nchimbi kiasi cha kupelekea kuvunja ndoa yao  na wivu uliomfanya afanye maamuzi ya kumuua mwenye mke ili apate nafasi ya kuwa huru na mke wa Nchimbi.

Aidha Kamanda Maigwa ametoa wito kwa watu wenye uhasama kupeleka matatizo yao katika vyombo vya usuluhishi badala ya kujichukulia maamuzi ambayo yanagharimu maisha ya watu na kuishia jela.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger