5/11/2021

Kimenuka : Shaffih Dauda Amshukia Haji Manara "Dunia yake ya ujanja Ujanja imefeli"


Reposted from @shaffihdauda_ The opposite of love is not hate, it's indifference, the opposite of art is not ugliness, it's indifference, the opposite of faith is not heresy, it's indifference, and the opposite of life is not death, it's indifference, mwenye kuelewa basi aelewe

Huyu Mtu wa kuitwa Haji Manara kuna dunia yake anayoishi akiamini ni dunia salama sana, lakini dunia hiyo ya ujanja ujanja kwa Watu waelewa wanaelewa ni dunia ndogo ya kawaida, dunia ya mbio za sakafuni kuishia ukingoni

Kwanza watu watofautishe kati ya Haji kama Muajiriwa wa Simba anayewakilisha Msimamo wa Simba eidha kimaandishi au Matamko, huyo sisi hatuna shida nae ila kuna Haji yule binafsi anaewakilisha mawazo yake binafsi kama mdau au Shabiki,huyu ndie Haji ninayemzungumzia hapa

Nimeisikiliza sauti yake ya kwanza kisha sauti yake ya pili, mara zote Haji akishayakoroga anajitahidi kuhusisha Simba na Mashabiki wa Simba, hii ndio dunia yake ya ujanja ujanja, lakini anasahau hizo Takataka anazoita zina familia ambazo wengine ni Mashabiki wa timu hiyo anayofanyia kazi

Unaweza kuniita Dauda takataka, Edo Kumwembe, Alex Luambano,Maulid Kitenge,Oscar na Vijana wadogo wanaochipukia ila hujui kuwa wana familia zao wanazozilipia tiketi, kununua jezi za Simba na kwenda uwanjani kuipa support Simba? Kauli yako ina madhara sehemu nyingi

Dunia yake ya ujanja Ujanja imefeli kutambua kuwa Haji huyu wa pili mwenye matamko yasiyo na busara yanaweza kuathiri hata taswira ya Haji kama Taasisi, mimi nasimama kuwasemea Wanahabari wote ambao ni Wahanga wa kauli chafu za Mtu huyu

Chanzo kikuu ni Wanahabari kuikosoa Press Release, lakini ni mara ngapi Haji huyo anasema vibaya kwa klabu zingine ambazo yeye anazijua na Watu hawajibu anavyojibu, Wanahabari wamesimama kwenye hoja, yeye ipi hoja yake

Yanga na Mashabiki wake wamekuwa wahanga wa kauli zake kwa kigezo cha utani wa jadi, Wanahabari wamekuwa wahanga wa kauli zake kutokana na taaluma zao, huyo ni Mtu mmoja wakuitwa Haji Manara, anaishi kwenye dunia gani?

Mwisho wa siku kirahisi unasema kuna Wanahabari umewalenga, wataje kwa majina na uwasafishe wengine, jitahidi sana kuishi smart na kuzingatia profession, Simba kama Taasisi wakutazame upya, ipo siku utakuja kuchafua zaidi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger