.

5/27/2021

Kocha Mkuu wa Yanga ataka makombe mawili yatue Jangwani
Kocha Mkuu wa Yanga, Nassreddine Nabi ameweka wazi kuwa wanahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na ule wa Kombe la Shirikisho.
Yanga katika Kombe la Shirikisho imetinga hatua ya nusu fainali baada ya ubao wa Uwanja wa Kambarage,Shinyanga kusoma Mwadui 0-2 Yanga 

Ndani ya Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 na kinara ni Simba mwenye pointi 61 amecheza mechi 25.

Nabi amesema:"Malengo yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na ule wa Kombe la Shirikisho hilo lipo wazi na tupo tayari kwa ajili ya ushindani, ".

Bingwa mtetezi wa mataji yote hayo mawili ni Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes naye ameweka wazi kuwa anahitaji mataji hayo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger