Kocha: Simba Ilijiandaa Kuiangamiza Yanga

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa, amefunguka kuwa amesikitishwa na tukio lililotokea juzi Jumamosi katika mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kuwa wao walijipanga vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

 

Gomes ametoa kauli hiyo kufuatia Yanga kugomea mchezo huo ambao awali ulipangwa kupigwa saa 11 jioni kabla ya kubadilishwa muda kwenda saa moja usiku hali iliyosababisha kuzuka kwa tafran.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa hakufurahishwa na tukio hilo kwa kuwa limewaumiza mashabiki wa soka nchini kwani hakuna aliyetegemea mchezo huo usingekuwepo tena.

 

“Binafsi naona halikuwa jambo zuri na hakuna ambaye amelifurahia kuanzia kwa mashabiki na wengine katika mchezo wa soka lakini matumaini yetu wahusika watajua nini cha kufanya na kwa wakati gani.

 

“Lakini nje ya hapo tulikuwa tumejiandaa vizuri kwa mchezo wetu na Yanga, wachezaji walikuwa kwenye morali kubwa ya mchezo lakini maamuzi yaliyotokea ndiyo yamekuwa tatizo kwa kuwa yameumiza wengi,” alisema Gomes.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE