.

5/27/2021

Kocha wa Simba ataja siri yakuendeleza vipigo


Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa licha ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini anajivunia kuona ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi chake jambo ambalo linafanya kikosi cha timu hiyo kuwa bora.
Simba imekuwa na wakati mzuri msimu huu katika michuano mbalimbali wanayoshiriki, ambapo wamefanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kuondolewa na Kaizer Chiefs Jumamosi iliyopita.

Jana Jumatano, kocha huyo aliiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye robo fainali nyingine ya kombe la Shirikisho (FA), ambapo walicheza dhidi klabu ya Dodoma Jiji.

Akizungumzia hilo, Gomes alisema: “Najivunia ubora wa kikosi nilichonacho na kile ambacho tumekifanya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu licha ya kutolewa, nafurahi kuona kuna ushindani mkubwa wa namba miongoni mwa wachezaji wangu jambo ambalo linatufanya tuzidi kuwa bora.

“Kila mchezaji anajituma sana mazoezini kuhakikisha anapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza, unaweza kuliona hili kupitia ubora unaoonyeshwa na wachezaji wetu hata wale wanaoingia kuchukua nafasi za wachezaji wanaoanza mara kwa mara.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger