5/07/2021

Kocha Yanga: Hatuna hofu na Simba
NASSREDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anatambua kwamba timu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ni timu nzuri ila hana hofu kuelekea mchezo wa kesho Uwanja wa Mkapa.
Nabi kesho atakutana na Gomes wa Simba katika mchezo wa Kariakoo Dabi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 hivyo kesho utakuwa ni mchezo wa kukata na shoka kwa timu zote mbili kuwania pointi tatu.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili imekusanya pointi 57 na Simba ipo nafasi ya kwanza imekusanya pointi 61.

Nabi amesema:"Ninaitambua Simba, nimewahi kukutana nao kwenye Ligi ya Mabingwa hata kocha wao Gomes, (Didier) ninamtambua.

"Licha ya kwamba Simba ni timu kubwa sina hofu nao nina amini kwamba kila timu ina mbinu zake na aina ya kufanya katika kutafuta matokeo," amesema. 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger