.

5/23/2021

Lady Gaga "Nilibakwa na Producer Wangu Nikiwa na Miaka 19 na Kupata Ujauzito"


Mwimbaji Lady Gaga amewasemea wasanii wa Kike ambao hukutana na changamoto kwenye kiwanda cha muziki, changamoto ambazo huwafanya kukata tamaa na kuacha muziki.

Lady Gaga amefunguka mazito ambayo yaliwahi kumkuta kipindi anaanza muziki, amesema alipata ujauzito akiwa na umri wa miaka 19 kufuatia kubakwa na aliyekuwa mtayarishaji wake wa muziki. Kwenye mahojiano na kipindi cha "The Me You Can't See" cha Oprah na Prince Harry, Gaga alisema
-
"Nilikuwa na umri wa miaka 19, na tayari nilikuwa nimeingia kwenye biashara ya muziki. Siku moja mtayarishaji aliniambia nivue nguo zangu zote. Nilikataa na kuondoka. Waliniambia kwamba wataenda kunibania kwa kuzuia nyimbo zangu zote. Waliendelea kunisumbua na kuniomba ngono na baada ya hapo... Sikumbuki hata."
-
Licha ya kuwa muungaji mkono wa kampeni ya #Metoo Lady Gaga amesema kwa sasa hana ubavu wala hamu ya kukutana na mtayarishaji yule aliyembaka kwa sababu mfumo wa muziki umekaa kionevu na hatari sana.
-
"Kwanza, nilihisi maumivu makali mno. Nilipatwa na ganzi. Kisha niliumwa kwa wiki na wiki. Na nilibaini yalikuwa ni maumivu yale yale niliyosikia siku ambayo yule mbakaji aliponitupa nje ya nyumba yetu nikiwa mjamzito kwa sababu nilikuwa naumwa sana na kutapika. Nilinyanyaswa, nilifungiwa studio kwa miezi." alisimulia Lady Gaga ambaye mwaka mmoja baadaye alipatwa na tatizo la afya ya akili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger