.

5/22/2021

Machifu wamuonya Chalamila


Kiongozi wa mila mkoani Mbeya ,Chifu Rocket Mwanshinga amemwonya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila kuwa makini na kutumia umri wake vizuri wakati huu anapokwenda kuongoza wakazi wa mkoa wa Mwanza.


Mwanshinga amesema leo  Ijumaa Mei 21,2021 katika ukumbi wa Mkapa jijini hapa wakati wa makabidhiana ofisi baina ya mkuu wa mkoa mpya Juma Homera ambaye anachukua nafasi ya Chalamila aliyehamishiwa Mwanza."Chalamila kafanye kazi kwa tahadhari Mwanza ni kubwa na ni ya tatu kwa ukumbwa nchini hivyo, ukatumie akili nyingi kwenye uongozi wake kwani Rais Samia Suluhu Hassan amekuamini," amesema.Pia, Chifu Mwanshinga amemuahidi Homera kuwatumia machifu katika masuala mbalimbali kwa kuwa, wanafahamu namna ya kudhibiti mambo.Amesema Mbeya umekuwa na changamoto  ya matukio mbalimbali yakiwemo watoto kuzimia shuleni jambo ambalo, amesema wamelidhibiti kikamilifu na sasa hali ni shwari.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger