.

5/20/2021

Majaliwa: Magazeti Manne tu Yaliyofungiwa
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Magazeti ambayo yamefungiwa kisheria Nchini Tanzania ni manne ambayo ni Mawio, Mseto, Mwanahalisi na Tanzania Daima ambapo hatua kadhaa zinaendelea ndani ya Serikali ili kuyafungulia magazeti hayo.

 

“Ninachofurahi ni kwamba hadi leo hii hakuna Redio hata moja au TV iliyofungiwa isipokua Online TV moja, Radio ni moja ilikua Wasafi FM wakati fulani lakini tukawaambia wafanye mapitio na sasa inaendelea na kazi.

 

“Magazeti manne yaliyofungiwa hatua zinaendelea ili warejee kwenye uandishi wao, kwa kuwa yalifungiwa kwa mujibu wa sheria basi sheria zilezile zitafata utaratibu wake kwa maelekezo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, hiyo ndio nia nzuri, nia njema ya Serikali yetu.

 

“Kwa miongozo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan hatudhani kama kutakua na jambo gumu lakini pia ni muhimu nasi tukaendelea kuheshimu kanuni, taratibu na sheria tulizonazo katika kufanya kazi yetu.” amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo akiongea na Jukwaa la Wahariri.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger