Makamu wa Rais akemea ulevi na uzinzi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema ili kiongozi awe mzuri ni lazima awe na sifa mbili ambazo ni Hodari wa kazi na mfano wa tabia nzuri na sio kuwa mlevi na mzinzi.
''Sitarajii kama hatutachapa kazi, sitarajii kwamba mtakuwa walevi kati yenu, sitarajii kuwa tutakuwa na orodha ya wazinzi na mengine maovu katika jamii yetu'' - Dkt. Mpango, Makamu wa Rais.

Ameongeza kuwa, ''Kiongozi mzuri ni lazima awe na sifa mbili, Hodari wa kazi na awe mfano kwa tabia, viongozi ambao mmepewa dhamana leo na wale waliopo ni muhimu sana tusiende kwenye vituo vyetu vya kazi tukawa mfano mbaya na tusichape kazi kwenye nchi masikini kama yetu.''

Pia amewasisitiza kuwa wakasaidie kukuza uchumi katika maeneo yao lakini wasiwe kero kwa wananchi bali wakafanye maamuzi mazuri kwa mambo wanayoyataka wananchi.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE