Makamu wa Rais Dr. Mpango atembelea kaburi la Magufuli

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, leo amezuru kaburi la aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli, mjini Chato mkoani Geita.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, alipozuru kaburi la Hayati Dkt. John Magufuli

Dkt. Mpango amezuru kwenye kaburi hilo akiwa njiani kuelekea Kibondo, mkoani Kigoma kwa ajili ya kufunga kampeni za uchaguzi katika jimbo la Muhambwe.

Hayati Dkt. John Magufuli, alifariki dunia Machi 17, 2021, katika hospitali ya Mzena Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo na alizikwa Machi 26 mwaka huu kijijini kwake Chato

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE