.

5/27/2021

Mama aibiwa mtoto hospitali, aeleza mazingira
Mtoto David Mfambo mwenye umri wa siku saba ameibiwa katika hospitali ya wilaya ya Frelimo mkoani Iringa, baada ya Mama mzazi kurubuniwa na mwanamke asiyemjua aliyemdanganya kwamba amshikie mtoto wake na kisha yeye kumuagiza akamchukulie kitu nje na aliporudi hakumkuta.
Akisimulia tukio hilo Mama mzazi wa mtoto huyo anayeitwa Dominita Kana, amesema kuwa mwanamke huyo aliyemwibia mwanaye walikutana mapokezi wakati Dominita akijianda kutoka kwenda kununua dawa ya mwanaye.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire, amesema kuwa taarifa za tukio hilo wanazo na ameiomba jamii kutoa ushirikiano endapo wataona mazingira ya mwanamke mwenye mtoto ambayo haeleweki ikiwemo mtoto kulia sana.

OPEN IN BROWSER
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger