Mama Anna Mghwira 'Kuna Uzembe Ulifanyaka Hospitali Kifo cha Mama Mzazi wa Hoyce Temu'


Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kilimanjaro, amesema watoa huduma wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC wamefanya uzembe katika tukio la kifo cha mama mzazi wa mtangazaji wa kipindi cha Tanzania Yetu, Hoyce Temu baada ya eneo la mapokezi kushindwa kuchukua hatua za haraka kuokoa uhai wake.

Akitoa kauli hiyo wakati wa ibada maalum ya mazishi kama rafiki wa karibu sana wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mnazi Mmoja Mkoani Kilimanjaro, Mama Mghwira alitoa kauli hiyo wakati akitoa neno la shukrani kwa maisha ya marehemu Sion Temu na kuwaasa watoa huduma wa KCMC kuzingatia utu na uadilifu katika kazi zao.

Mama Anna Mghwira aliongeza kuwa kulikuwa na uzembe baada ya mgonjwa kufika hapo na kukaa kwa zaidi ya masaa mawili bila kupokelewa katika mapokezi hiyo ya wagonjwa KCMC.


Aidha, Mama Anna Mghwira alitumia wasaha huo kwa wana Kilimanjaro kujiandaa kumpokea Mkuu wa Mkoa mpya kama walivyompokea yeye na kukaa kwa miaka minne ndani ya Mkoa huo.


Marehemu mama Sion Temu alifariki dunia Jumapili ya siku ya Mama duniani (Mother’s Day) dakika chache baada ya kuongea na binti zake kwa simu na kuwatakia heri ya siku hiyo na kuzikwa siku ya Jumamosi tarehe 15/5/2021 nyumbani kwake Moshi Mnazi Mmoja mkoani Kilimanjaro.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE