5/16/2021

Manara Afugunguka Baada ya Kuchapwa Bao 4 "TUMECHEZA HOVYO, TUMEADHIBIWA"

 BAADA ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa FNB Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa walicheza hovyo.

Kichapo hicho kinakuwa cha kwanza kwa Kocha Mkuu Didier Gomes kushuhudia idadi kubwa ya mabao kwa timu yake ikifungwa akiwa katika benchi baada ya kupokea mikoba ya Sven Vandenbroeck.


Haji Manara kupitia Ukurasa wake wa Istagram alisema:" Alhamdulillah. Tumefungwa na aliye bora usiku wa leo, tumecheza hovyo na tumefanya makosa mengi yaliyostahili adhabu hii.
"Life go on, (maisha lazima yaendelee) na still, (bado) tunazo dk tisini nyingine za kuamua,".
Mchezo wa robo fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ambapo Simba wanapaswa kufunga mabao zaidi ya manne ili kusona mbele hatua ya nusu fainali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger