Maua Sama: Wasanii Msitufokee!

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amewataka wasanii wenzake waache mikwara kwenye kazi.

 

Akizungumza na MIKITO NUSUNUSU, Maua ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ya Wivu aliyofanya na Aslay, amesema kuwa unakuta msanii anaposti hata yupo nchi za nje na msanii mkubwa na kusema kolabo inakuja halafu unashangaa mwaka mzima hola.

 

“Wasanii jamani tuwe tunapunguza mikwara tutakuja kuuana kwa presha kwa kweli maana unakuta msanii anaposti hata yupo na msanii wa nje ya nchi anaandika kolabo ipo njiani kubwa ni wamepiga picha tu,” alisema Maua.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE