Mbunge Ataka Kupanda Juu ya Meza Bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





MBUNGE wa Viti Maalum (CCM),  Jacqueline Msongozi ameomba kupanda juu ya meza akiwa kwenye ukumbi wa Bunge ili kuieleza dunia kuwa wakulima hawataki mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye mazao madogo ikiwemo ufuta.

 

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo mwaka 2021/22 jana Jumanne Mei 25, 2021, Msongozi amesema mfumo huo haufai kwa mazao madogo.

 

Amebainisha kuwa wakulima wa Ruvuma wanalima ufuta kwa ajili ya kujikimu lakini kupitia mfumo huo hutakiwa kupeleka mazao katika mfumo wa stakabadhi ghalani  na kukopwa  jambo  linalosababisha wakose fedha za kugharamia mahitaji yao.

 

“Spika (Job Ndugai) niruhusu nipande juu ya meza, niruhusu nipande juu ya meza sasa hivi,” amesema Msongozi  na Ndugai kulazimika kumtuliza akisisitiza kuwa leo kitaeleweka kuhusu mfumo huo.

 

“Usipande mheshimiwa Jacqueline kwa sababu lazima leo kieleweke hapa kuhusiana na mfumo wa stakabadhi ghalani,” amesema Spika Ndugai.

 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad