Mbunge: Wanaume Wanajadili Sana Kuhusu Simba na Yanga Kuliko Afya zao


Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Mchafu, amesema kama nguvu zaidi ingetumika kujadili masuala ya #Afya ikiwemo kupima VVU, huenda vita dhidi ya Ugonjwa huo ingekuwa nyepesi

Ameongeza "Wanaume wa #Tanzania wanatumia muda mwingi kujadili Usimba na Uyanga, hawapimi VVU na hawataki kupima, hivi ingetumika muda huo kuzungumza masuala ya kupima Afya zao si tungeshinda"

Akieleza zaidi, amesema tatizo lipo kwa Wanaume waliooa ambao hutegea Wake zao wapime ndio nao wapate majibu na kujipa matumaini wakati kinga za mwili zinatofautiana.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE