5/11/2021

Metacha Mnata Kupewa Mkataba Mpya

 


KIPA namba moja wa Yanga, Metacha Mnata inaelezwa kuwa anaandaliwa mkataba mpya ili aweze kusaini dili jipya.

Nyota huyo hivi karibuni ilielezwa kuwa anahitaji kusepa ndani ya Yanga kutokana na kutuhumiwa kwamba anacheza chini ya kiwango jambo ambalo lilimkasirisha nyota huyo.

Mechi ambayo ilileta utata ni ile ya sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania ambapo ilikuwa ni Fiston Abdulazack alianza kufunga bao la Polisi Tanzania likafungwa dakika za lala salama na kuwafanya Yanga kugawana pointi mojamoja.

Suala hilo lilifanuliwa na Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla kwamba hawakuwahi kumtisha hivyo yalikuwa ni maneno ambayo hayana ukweli.

“Mnata, (Metacha) kwa sasa anaweza kupewa mkataba mpya kwa kuwa hakuna tofauti ambazo zipo, ni kwamba mkataba wake upo ukingoni ila maboresho yatafanyika,” ilieleza taarifa hiyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger