Miili yapatikana imezikwa karibu na mto nchini India

Miili kadhaa imekutwa imezikwa katika mchanga kwenye Mto Ganges [gan·jeez] kaskazini mwa India, siku chache baada ya miili ya watu wanaodaiwa kuambukizwa virusi vya corona kukutwa ikielea kwenye maji. 
Vyombo vya habari vya India vimeripoti kuwa tangu wimbi la pili la COVID-19 lilipozuka na kusababisha ongezeko la vifo nchini humo, gharama za kuchoma maiti zimepanda.

 Inaelezwa kuwa hali hiyo inaweza kuwa imechangia kwa familia masikini ama kuzitupa maiti kwenye mto au kuzizika. 

Miili mingi iliyokuwa imefunikwa kitambaa ilikutwa jana imezikwa kwenye mto katika maeneo mawili ya wilaya ya Unnao iliyoko jimboni Uttar Pradesh. 

Takriban miili 100 ilisombwa na maji katika kingo za Mto Ganges kwenye wilaya za karibu katika jimbo la Uttar Pradesh na Bihar, mapema wiki hii.

 Katika wimbi la sasa la maambukizi, India inarekodi takriban visa 350,000 na vifo 4,000 kwa siku.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE