Mondi, Zari WamerudianaMjini kuna mambo! Hivi karibuni msanii mkubwa wa muziki wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliposti picha akiwa akiwa kwenye pozi la kimahaba na zilipendwa wake Zarinah Hassan ‘Zari the boss lady’ jambo lililozua maswali mengi huko mjini Instagram.

Miongoni mwa maswali ambayo watu wengi walikuwa wanajiuliza ni kwamba je? Wawili hao tayari wamesha rudiana? Lakini mpaka sasa bado haijathibitika licha ya kwamba kaka mkubwa wa staa huyo Romy Jons tayari ameshaanza kujiita kuwa yeye ni shemeji wa Zari.

STORI NA MEMORISE RICHARD

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE