Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mrithi wa mfalme wa Wazulu utata mtupu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMzozo kuhusu ni nani atakayemrithi marehemu Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini, sasa unaelekea mahakamani, vyombo vya habari vinaripoti.Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kadhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini

Mke wa kwanza, Malkia Sibongile Dlamini, anapinga kutekelezwa kwa wosia wa mfalme uliomtaja mfalme ajaye – huku kukiwa na madai kwamba wosia wake wa mwisho huenda ulighushiwa.

Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kadhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu.

Alikuwa ameteuliwa kushikilia wadhifa huo tarehe 24 mwezi Machi baada ya Mfalme Zwethilini kufariki kutokana na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari akiwa na umri wa miaka 72.

King Zwelithini's wife 'demands 50% of estate' | Witness

Lakini katika kesi ya kupinga uteuzi wa Malkia Mantfombi kama mrithi wa Mfalme, Malkia Sibongile alitaka mahakama kutambua ndoa yake na na marehemu mfalme huyo kuwa halali. Pia anataka kupewa asilimia 50 ya usimamizi wa nyumba zake.

Siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Zulu Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi alielezea hatua hiyo ya kisheria kama “aibu”, alipokuwa akizungumza na Shirikala utangazaji la Afrika Kusini SABC.

“Baadhi ya wanafamilia wa kifalme wameshangazwa sana na kile alichofanya kwasababu bado anaomboleza. Wao, kama wajane wa Mfalme, na hatua ya kukimbilia mahakamani kwa njia waliofanya ni fedheha kwa familia ya ufalme.” aliambia SABC.


Post a Comment

0 Comments