Mtumishi Wa Serikali Ahukumiwa Miaka 200 Jela

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Leo tarehe 07/05/2021 Mahakama ya wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe imemhukumu ndugu SEMENI GWEWA MSWIMA (Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mlowo) Kifungo cha miaka 200 au kulipa faini ya Tshs.52,000,000/= pamoja na kurejesha kiasi cha Tshs.30,850,000/= alichoiibia Halmashauri wilaya ya Mbozi.

Kesi hiyo ambayo ni Kesi ya uhujumu Uchumi Na.01/2021 ilifunguliwa leo na TAKUKURU Mkoa wa Songwe mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mh.Vitalis Changwe ambapo Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa sitini(60) ambapo ndani yake kuna makosa ya kutumia nyaraka za uwongo kinyume na vifungu vya 342 na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2019 na makosa ya wizi kwa Mtumishi wa Umma kinyume na vifungu vya 258(1) na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Mwaka 2019.Akisomewa Mashtaka hayo,



Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe Bwn Emanuel Ndembeka akisaidiana na Bi.Simona Mapunda,alieleza mahakamani hapo kwamba Mshtakiwa kwa tarehe tofauti tofauti kati ya tarehe 04/07/2019 hadi tarehe 08/05/2020 kwa kutumia hati za malipo na hundi zilizoghushiwa aliweza kutoa na kuiba fedha jumla ya Tshs.30,850,000/= toka katika akaunti Na.61210014674 ambazo ni mali ya Halmshauri ya wilaya ya Mbozi.



Mshtakiwa alikiri makosa yote 60 yaliyokuwa yakimkabili.

 

Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Changwe alimwamuru Mshtakiwa kulipa faini ya Tshs.800,000/= au kwenda jela miaka mitatu(3) kwa kila kosa la kuwasilisha nyaraka za uwongo,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa arobaini(40).



Hakimu huyo pia alimwamuru Mshtakiwa alipe faini ya Tshs.1,000,000/= au kwend jela miaka minne(4) kwa kila kosa la wizi kwa Mtumishi wa Umma ,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa ishirini(20).Pamoja na kulipa faini hizo,Mahakama ilimwamuru Mshtakiwa ajereshe katika halmashauri husika fedha alizoiba kiasi cha Tshs.30,850,000/=.Mshtakiwa alishindwa kulipa fedha.

Na Dicksoni Kapungu, Songwe

L
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad