Nabi Ashikilia Hatma ya Fiston, Shikhalo Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WAKATI baadhi ya mastaa wa kikosi cha Yanga wakitarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, uongozi wa Yanga umesema kwamba, hatma ya wale ambao wataongezewa mikataba, ipo chini ya kocha wao, Nasreddine Nabi.

 

Baadhi ya wachezaji wa Yanga wanaotarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu ni Saidi Makapu, Deus Kaseke, Faroukh Shikhalo, Metacha Mnata na Fiston Abdoul Razack.

 

Nabi raia wa Tunisia, amekabidhiwa kikosi hicho Aprili 20, mwaka huu ambapo anatarajiwa kuisuka upya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ambapo wana asilimia kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.



Akizungumza na Spoti Xtra, Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Thabit Kandoro, alisema: “Wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu, suala lao tayari lipo katika kamati ya usajili.

 

“Kwa sasa tunasubiri ripoti ya kocha mkuu kama atawahitaji kwa msimu ujao basi wataongezewa mikataba, hivyo yeye ndiye atakayeamua hatma yao kutokana na viwango vyao mazoezini na kwenye mechi.

 

“Kocha Nabi kwa sasa anaandaa kikosi sio kwa ajili ya michuano ya ndani tu, bali kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambayo tunaweza kushiriki msimu ujao.”

LEEN ESSAU, Dar es Salaam
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad