Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Namungo Wanogewa Kimataifa

TIMU ya Namungo imeondoka jana kuelekea jijini Dodoma kumenyana na JKT Tanzania katika mchezo wa michuano ya shirikisho huku wakiwa na malengo ya kuiwakilisha tena Tanzania kimataifa.

 

Namungo kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi.

 

Mchezo wa mwisho uliopigwa Aprili 28, mwaka huu Cairo nchini Misri dhidi ya Pyramids, Namungo ilipoteza kwa bao 1-0 lililofungwa na Ibrahim Adel dakika ya 65.Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Namungo, Kindamba Namlia alisema: “Timu imerejea salama kutoka Misri baada ya kumalizika kwa mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Pyramids.

 

“Tutaondoka na jumla ya wachezaji 26 kuelekea Dodoma ambapo tunatarajia kucheza kwa kufa au kupona ili tupate nafasi nyingine ya kuiwakilisha nchi kwa msimu ujao.“Licha ya kupoteza michezo yote lakini tumepata uzoefu mkubwa ambao utatusaidia kwa msimu unaokuja,” alisema Kindamba.

STORI NA LEEN ESSAU

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments