Nay wa Mitego "Kuanzia KESHO Najitoa Basata, Nitaanza Kufanya Mziki Mtaani"


 Star wa muziki nchini 🇹🇿 @naytrueboytz ametangaza kuwa kuanzia siku ya kesho May,6 ataanza kufanya taratibu za kujitoa uanachama wa #Basata, kufuatia sheria yao mpya ya kuzipitia nyimbo za wasanii kabla ya kuzipeleka kwenye vituo vya redio na Tv

#NayWaMitego amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa instagram akiandika ujumbe ulioashiria kuilaani sheria hiyo mpya

"Kuanzia Kesho Nitakua Nafanya Taratibu Za Kujitoa Uanachama Wa Basata, Kufuatana Sheria Yao Mpya Sitopeleka Wimbo Wangu Wowote Radioni Coz Hautakua Na Kibali Chochote Cha Kupigwa Redioni Kama Sheria Inavyotaka. Nitafanya Mziki Wangu Mtaani.#RaisiWaKitaa" ✍️ .. @naytrueboytz

 

#ThisIsAfrica #AfricaIsWatching

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE