Nisha Atamani Kuolewa na Dimpoz

advertise here
Unaambia picha ya Ommy Dimpoz imemfanya msanii wa filamu Nisha Bebe kutamani kuolewa na msanii huyo wa muziki wa BongoFleva ambaye kwa sasa yupo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kuhiji.

 

Nisha Bebe amesema Ommy Dimpoz amefanya kitu kikubwa sana na amemshawishi na yeye kwenda kufanya tukio hilo la kuhiji Mjini Mecca, Saudi Arabia kama alivyokuwa anafanya marehemu Mzee Majuto.

 

“Yaani sijawahi kuona picha ya mtu nikatamani kuolewa naye, mara baada tu ya kuiona hii picha nimetamani kuolewa na Ommy Dimpoz na ni kitu ambacho hata akilini mwangu hakikuwepo,umefanya kitu kikubwa sana.”

 

“Serious wa kwanza kunishawishi kutamani kuhiji ni marehemu baba yangu Mzee Majuto, Ommy leo umenikumbusha vitu vingi sana, kiukweli nimejiskia raha kutoka moyoni kwa hiki ulichofanya” ameongeza.

 

Pia, amemtaka Ommy Dimpoz asirudie makosa aliyowahi kuyafanya na aendelee kuishi kwenye mstari ulionyooka mpaka mwisho wa maisha yake.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE